Watu 3 Wamenusurika Moto Mkubwa Bariadi

Watu watatu wa mtaa wa Kidinda, wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamenusurika kifo baada ya nyumba yao ya makazi kuwaka moto.

Aidha chanzo cha moto huo kimetajwa kuwa hitilafu ya umeme, huku nyumba yenye vyumba vitano ikiteketea kiasi cha vyumba viwili.

Joyce Komba na Elizabeth Daniel wamesema kuwa mbali na vyumba vilivyoteketea, moto umeharibu magodoro, vitanda na mali nyingine zilizokuwa ndani ya nyumba ambapo  Wote  hao wamenusurika baada ya kutoka nje mapema.

Moto huo ulianza katika chumba cha watoto na ulizimwa kwa ufanisi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Mashuhuda wa tukio, Kija Bulenya na Rahel Godwin, wamesema waliona moshi ukienea juu ya madirisha na waliposifika eneo la tukio, walihisi sauti za kuomba msaada kutoka kwa familia iliyokumbwa na moto.

Hata hivyo Kaibu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, Faustin Mtitu, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanakagua miundombinu ya umeme kila baada ya miaka mitano ili kuzuia ajali zinazotokana na hitilafu za umeme. 

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii