Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa (kulia) akioneshwa picha zilizopo ukutani ( Wall Museum) zilizokuwa zikimuonesha historia ya Mgodi wa Geita Gold Mining Limited (GGML) kutoka kwa Makamu wa Rais wa kampuni mama ya GGML, AngoGold Ashanti, anayehusika na Uendelevu na Mahusiano barani Afrika, Bw. Simon Shayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya mgodi huo hapa nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa (kati kati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa mgodi wa dhahabu wa Geita ( Geita Gold Mining Limited-GGML) wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya uwepo wa mgodi huo hapa nchini zilizofanyika Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Dkt. Steven L. Kiruswa, Naibu Waziri wa Madini, akipokea kitabu cha kumbukumbu (legacy book) kilichoandaliwa kuadhimisha miaka 25 ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kutoka kwa Lizelle Marwick, Afisa Mkuu wa Sheria wa AngloGold Ashanti na Mwenyekiti wa Bodi ya GGML, wakati wa hafla ya gala ya maadhimisho ya miaka 25, iliyofanyika Hyatt Kilimanjaro, Dar es Salaam.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime