Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe Said Mtanda, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina baada ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nenge Jonathan Paul kuvuliwa cheo na kushushwa kuwa mwalimu wa kawaida kwa madai ya kushindwa kusimamia ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Bugumangala iliyopo wilayani Magu, mkoani.
Mtanda ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake wilayani Magu, baada ya kubaini kuwa mwalimu huyo alichukuliwa hatua ya kinidhamu bila kuwepo kwa uchunguzi wa kina unaoonesha kama alihusika moja kwa moja katika dosari zilizojitokeza kwenye usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo Mwalimu Mkuu huyo alitendewa haki au la katika hatua iliyochukuliwa dhidi yake.
Amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji wa pamoja katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, akieleza kuwa jukumu hilo halipaswi kubebwa na mtendaji mmoja pekee, bali ni wajibu wa wadau wote kuanzia ngazi ya chini hadi juu.
Aidha Mh Mtanda ameongeza kuwa usimamizi wa ujenzi wa miradi ya maendeleo unahusisha watendaji mbalimbali, wakiwemo Afisa Elimu, Mhandisi wa Halmashauri pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Florencia Peter tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime