VISIWA VYA BEZI NA TEFU KUNUFAIKA NA UMEME WA JUA MWANZA

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mhe. Kafiti William Kafiti amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanzisha mradi wa kusambaza umeme wa mfumo wa jua majumbani (Stand Alone Solar Home System) katika maeneo ya visiwa, ambapo kwa Wilaya ya Ilemela, visiwa vya Bezi na Tefu ni miongoni mwa wanufaika. 


Amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi katika Kata ya Kayenze kwa alipotembelea katika visiwa vya Tefu na Bezi, akiwa ameambatana na Mhandisi Miradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mkoa wa Mwanza Mhandisi Awesa Mnunduma
pamoja na Diwani wa Kata ya Kayenze Mhe. James Katoro Mwanaweya.

Ameeleza dhamira yake ya kuboresha huduma za kijamii kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa zahanati katika Kisiwa cha Tefu, ujenzi wa zahanati ya Bezi, ujenzi wa tanki la maji kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa Kisiwa cha Bezi, pamoja na ujenzi wa barabara na ufungaji wa taa za barabarani katika kisiwa hicho, hatua zitakazosaidia kuimarisha usalama na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake Mhandisi Miradi wa REA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Awesa Mnunduma amesema kuwa kwa mfumo wa Solar wa Watt 50, wananchi watalipia Tsh 105,000/= badala ya Tsh 420,000/=, sawa na ruzuku ya asilimia 75. Kwa mfumo wa Watt 80, wananchi watalipia Tsh 227,500/= badala ya Tsh 650,000/=, ikiwa ni ruzuku ya asilimia 65, huku mfumo wa Watt 100 wananchi wakilipia Tsh 315,000/= badala ya Tsh 700,000/=, ruzuku ikiwa ni asilimia 55.

Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji akiwa ni Evance Mlyakado usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa. Lakini pia tembelea tovuti yetu ya ,www.jembenijembe.com na mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz 

Na tunasema Asante kwa time

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii