waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesisitiza umuhimu wa kuharakisha utekelezaji wa mifumo ya zana endelevu za kilimo barani afrika kwa kuunganisha kikamilifu na sera,mikakati na mipango ya Kitaifa.
Dkt Mwigulu ameeleza hayo katika mkutano wa kwanza wa kikanda wa Afrika wa Matumizi Endelevu ya Zana za Kilimo uliofanyika leo jiji Dar es Salaam.
waziri mkuu ameeleza ulinganifu huo utaimarisha uratibu wa kikanda ,kuepusha mwingiliano usio wa wa lazima wa afua na kuhakikisha juhudi ambazo zitaleta mabadiliko halisi katika maisha ya wakulima.
Aidha ameeleza manufaa ya kutumia teknolojia za kidigitali katika upangaji wa uzalishaji ,utoaji wa huduma za zana za kilimo,usimamizi wa taarifa na ufuatiliaji wa matokeo ili kuhakikisha uwekezaji huo unapimika na wenye tija.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Florencia Peter tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime