Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata watu 19, wakiwemo madereva na makondakta wa daladala, kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya wizi dhidi ya abiria wanaotumia usafiri wa umma katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbroad Mutafungwa, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na operesheni maalumu iliyofanyika baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu kuongezeka kwa matukio ya wizi kwenye daladala.
DCP Mutafungwa amesema baadhi ya watuhumiwa walikuwa wakishirikiana na vibaka ili kuwaibia abiria kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo msongamano wa abiria na kubadilisha njia ghafla ili kuwachanganya.
Aidha ameeleza kuwa operesheni hiyo imehusisha maeneo yenye changamoto kubwa ya wizi, yakiwemo vituo vikuu na barabara zinazokuwa na idadi kubwa ya wasafiri.
Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kutoa taarifa mapema pindi wanapobaini vitendo vya uhalifu, huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea na ooperesheniili kuhakikisha usalama wa abiria unaimarika jijini Mwanza.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime