Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert John Chalamila, ameingilia sakata la ardhi katika eneo la Nyakasangwe, Wilaya ya Kinondoni, baada ya mwananchi Glory Munisi kudai kupoteza fedha zake katika mchakato wa ununuzi wa kiwanja.
Akizungumza eneo la tukio leo Februari 13 mwaka huu RC Chalamila amesema amepokea maelezo kutoka kwa pande zote zinazohusika na kubaini kuwa Munisi aliingia makubaliano ya kununua kiwanja, lakini baadaye akaingia kwenye mgogoro uliomwacha bila kupata haki yake.
Kutokana na hali hiyo, RC Chalamila ametoa maelekezo kwa mwenyekiti wa eneo husika kuhakikisha mwananchi huyo anarejeshewa fedha zake zote alizolipa katika mchakato huo.
Amesema Serikali imelenga kukomesha migogoro ya ardhi inayochochewa na uzembe au vitendo vya udanganyifu katika ngazi za mitaa, akisisitiza kuwa viongozi wanaopaswa kusimamia haki za wananchi hawapaswi kuwa chanzo cha migogoro.
Aidha, amewataka wananchi kuhakikisha wanafuata taratibu zote za kisheria kabla ya kufanya manunuzi ya ardhi, ikiwemo uhakiki wa umiliki na nyaraka halali, ili kuepuka hasara na migogoro isiyo ya lazima.
Sasa ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Benson Mwakakongole tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
Na tunasema Asante kwa time
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime