BoT Yaonya Matumizi ya Noti kama Zawadi za Valentine

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa onyo kali kwa wananchi wanaotumia fedha kama mapambo au zawadi wakati wa maadhimisho ya Valentine, ikisema tabia hiyo ni kinyume cha sheria na husababisha uharibifu wa noti.

Akizungumza jijini Dodoma, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amesema matumizi hayo yamekuwa yakiongezeka nyakati za sikukuu, hali inayochangia hasara kwa Taifa kutokana na uharibifu wa fedha.

Ameeleza kuwa noti zinazofungwa kwenye mashada ya maua au kubandikwa kwa gundi hupoteza ubora wake kutokana na mikunjo na kemikali zinazotumika, jambo linalozifanya zishindwe kutumika kwa muda mrefu.

Gavana Tutuba amesisitiza kuwa fedha ni mali ya Serikali na zinapaswa kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa kisheria, si kama mapambo au zawadi za maonesho.

BoT imewataka wananchi kutumia njia mbadala za kutoa zawadi, ikiwemo kununua bidhaa au kutoa fedha katika hali yake halisi bila kuziharibu.

ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda.#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii