Serikali Yekeza Bilioni 131 Kuimarisha Uzalishaji wa Vitambulisho vya Taifa – Katambi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 131 katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa lengo la kuboresha teknolojia na kuongeza kasi ya uzalishaji wa vitambulisho vya taifa.

Amesema uwekezaji huo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha huduma za utoaji wa vitambulisho zinawafikia wananchi kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa kupitia matumizi ya mifumo ya kisasa ya kidijitali.

Waziri Katambi ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika Makao Makuu ya NIDA jijini Dar es Salaam, ambapo alitembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji na usambazaji wa vitambulisho pamoja na kujionea maendeleo ya miundombinu ya kiteknolojia.

Aidha, ameipongeza NIDA kwa kutoa gawio la Shilingi bilioni 38 kwa Serikali Kuu, akisema hatua hiyo inaashiria usimamizi mzuri wa rasilimali za umma na kuimarika kwa utendaji wa taasisi hiyo.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuimarisha taasisi zake ili ziweze kutoa huduma bora, zenye tija na zinazochangia maendeleo ya Taifa.

Ili kupata undani wa  taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili  alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @jacobmlay__  tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.

Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii