Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Said Mtanda, ameagiza halmashauri zote zenye upungufu mkubwa wa madawati, ikiwemo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kwimba, Magu na Sengerema, kuanzisha karakana maalum za kutengeneza madawati ili kupunguza gharama na kuongeza kasi ya uzalishaji.
RC Mtanda ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya kukabidhi jumla ya madawati 2,939 kwa shule 13 za elimu ya awali na msingi ndani ya Jiji la Mwanza.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi kukaa chini darasani na kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Ameongeza kuwa ofisi yake itaanza kufanya ziara za ukaguzi ndani ya miezi mitatu ijayo ili kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo na kuhakikisha kila halmashauri inatekeleza kwa vitendo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kibamba, amesema wamejipanga kuhakikisha kuwa ifikapo Juni mwaka huu changamoto ya upungufu wa madawati katika Jiji la Mwanza inakwisha kabisa.
Amesisitiza kuwa katika kipindi chote cha mpito, hakuna mwanafunzi atakayelazimika kukaa chini kutokana na ukosefu wa dawati, huku akiahidi usimamizi madhubuti wa rasilimali na uzalishaji wa madawati kwa wakati.
Sasa ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kamili mchana ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Evance Mlyakado tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime