Tayari mshindani wake mkuu André Ventura amekubali kushindwa na mshindi anatarajiwa kuchukua madaraka Machi 9, akimrithi Rebelo de Sousa, ambaye ameiongoza nchi hiyo ya kusini-magharibi mwa Ulaya tangu 2016.
Mgombea wa mrengo wa kati wa kushoto António José Seguro ameshinda urais nchini Ureno katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo hapa jana, makadirio yameonyesha.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali RTP limeripoti kwamba asilimia 98 ya kura tayari zimehesabiwa na kwamba Seguro, kutoka Chama cha Kisoshalisti (PS), amemshinda mgombea mrengo wa kulia André Ventura, na kupata takriban 66% ya kura, .
Aidha akizungumza na waandishi wa habari baada ya matokeo ya awali , Seguro amewashukuru wareno kwa kumchagua na kusifu mchakato mzima wa uchaguzi na kwamba ulifuata misingi ya demokrasia.
Hata hivyo tayari mshindani wake mkuu André Ventura amekubali kushindwa na mshindi anatarajiwa kuchukua madaraka Machi 9, akimrithi Rebelo de Sousa, ambaye ameiongoza nchi hiyo ya kusini-magharibi mwa Ulaya tangu 2016.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime