Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mabadiliko ya viongozi aliowateua yamelenga kuimarisha mwelekeo wa utekelezaji wa shughuli za Serikali ili kwenda sambamba na kasi ya matarajio na mahitaji ya wananchi.
Rais Samia amesema hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini na kuhakikisha mipango yote ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati na kwa tija.
“Mabadiliko haya ni katika jitihada za kuendana na kasi ya utekelezaji, lengo ni kwenda na kasi ya matarajio au mahitaji ya wananchi,” amesema Rais Samia.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumatatu, Februari 9 mwaka huu Ikulu jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua Februari 6 mwaka huu.
Hata hivyo amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa weledi, uwajibikaji na kushirikiana kwa karibu na wananchi ili kutatua changamoto zao na kusukuma mbele maendeleo ya Taifa.
Kwa taarifa zaidi tufuatilie na usikilize jembe Habari Kamili hapo saa saba kumi kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni @ekadomaster20 tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime