Wapiganaji 27 wa Alshabaab wauliwa nchini Somalia

Wizara ya ulinzi ya Somalia imesema operesheni hiyo kubwa iliendeshwa kweye maeneo ya Lower Jubba na Jubba ya Kati, ambako walikamata silaha kadhaa pamoja na mabomu ya kutega ardhini.

Wizara ya ulinzi ya Somalia imesema kwamba vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo na vikosi vya usalama vya kikanda wamewauwa wapiganaji 27 wa kundi la Al Shabaab katika jimbo lenye utawala wake wa ndani la Jubbaland.

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kwamba operesheni hiyo imefanyika kwa ushirikiano wa kimataifa uliosadia kuendesha mashambulio ya anga, ingawa haikutaja mshirika wa kimataifa aliyehusika kutowa msaada huo.

Mapigano yaibuka Jubaland nchini Somalia

Wizara hiyo ya ulinzi ya Somalia imesema pia operesheni hiyo kubwa iliendeshwa kweye maeneo ya Lower Jubba na Jubba ya Kati, ambako walikamata silaha kadhaa pamoja na mabomu ya kutega ardhini.

Marekani imekuwa ikifanya mashambulio ya anga nchini Somalia ikidai kuisaidia katika mapambano dhidi ya al Shabab, kundi ambalo linafanya uasi kwa miongo miwili kujaribu kuipunduwa serikali kuu mjini Mogadishu.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii