Israel kupitia Baraza lake la Usalama, imepitisha hatua mpya zinazolenga kuimarisha udhibiti wake katika Ukingo wa Magharibi na kupunguza mamlaka ya Mamlaka ya Palestina.
Hatua hizo zimeongozwa na Waziri wa Fedha mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich, ambaye amesema zinalenga kurahisisha walowezi wa Kiyahudi kuwashinikiza Wapalestina kuachia ardhi, akisisitiza kuwa wanazidi “kuzika wazo la kuwepo kwa taifa la Palestina.”
Kwa mujibu wa uamuzi huo, mamlaka zaidi yatahamishiwa kwa Israel katika masuala ya ardhi, ujenzi na usimamizi wa maeneo yanayokaliwa, jambo linalotajwa kuongeza shinikizo kwa jamii za Kipalestina.
Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, amelaani hatua hizo akizitaja kuwa ni hatari na jaribio la kuhalalisha upanuzi wa makazi ya walowezi.
Amesema uamuzi huo unakiuka sheria za kimataifa na unatishia kabisa mchakato wa amani Mashariki ya Kati.
Aidha ametoa wito kwa Marekani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka kuzuia kile alichokiita kuendelea kwa uvamizi na kunyimwa haki kwa wananchi wa Palestina.
Hata hivyo hatua za Israel zinaendelea kukosolewa kimataifa huku wachambuzi wakionya kuwa zinaweza kuongeza mgogoro na machafuko katika eneo hilo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime