Rais Samia Kuapisha Viongozi Ikulu Leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Februari 09 mwaka huu anatarajiwa kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni katika hafla itakayofanyika Ikulu, Dar es Salaam kuanzia saa 05:00 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, viongozi watakaoapishwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Makatibu Tawala wa Mikoa, Naibu Makatibu Wakuu, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango pamoja na Mabalozi.

Ambapo sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya Rais katika kuimarisha ufanisi wa utendaji wa Serikali kupitia uteuzi wa viongozi wenye uwezo na uzoefu katika maeneo mbalimbali ya utawala.

Hata hivyo hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, wageni waalikwa pamoja na wadau mbalimbali, huku Rais akitarajiwa kutoa maelekezo muhimu kwa viongozi watakaoapishwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa wananchi.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii