KESI iliyofunguliwa na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Geoffrey Mwambe katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam akipinga kunyang'anywa hati yake ya kusafiria imesikilizwa leo.
Kesi hiyo namba 488 ya mwaka 2026 ilifunguliwa na Mwambe akipinga hatua ya Idara ya Uhamiaji kumnyang'anya hati hiyo.
Kupitia wakili wake Hekima Mwasipo Mwambe amefungua shauri hilo akiwashitaki Kamishna wa Jeshi la Uhamiaji pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai kuwa hatua hiyo imekiuka haki zake za kikatiba, ikiwemo haki ya kusafiri.
Wakili Mwasipo amedai mahakamani hapo kuwa kunyang’anywa kwa hati ya kusafiria kwa mteja wake hakukufuata taratibu za kisheria na hakukuwa na sababu za msingi zilizoelezwa wazi.
Kwa upande wao mawakili wa serikali waliiomba mahakama ipate muda wa kujibu madai hayo kabla ya kutoa uamuzi wowote.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime