Viongozi wa Ulaya kutunishiana misuli na Trump

Viongozi wa Ulaya wanashiriki Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) ambalo litafanyika mjini Davos wakati mvutano baina yao na mshirika wao wa kijadi Marekani ukizidi kufuatia kitisho cha Donald Trump kukitwaa kisiwa cha Greenland.

Ambapo tayari wajumbe wa Marekani walishawasili mapema kwenye kongamano hilo la ngazi za juu kuitetea ajenda hiyo ambayo imeutikisa mfumo wa kilimwengu unaoungwa mkono na WEF.

Hivyo mkuu wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa walitarajiwa kulihutubia jukwaa hilo siku ya Januari 20 sambamba na Waziri Mkuu wa China He Lifeng na Waziri Mkuu wa Kanada, Mark Carney ambao nchi zao pia zina mzozo mkubwa na Trump.

Hata hivyo Trump mwenyewe alitazamiwa kupanda jukwaani siku ya Jumatano na kisha kushiriki matukio mengine siku ya Alkhamis na tayari Ulaya ilishatangaza kuzingatia hatua za kulipiza kisasi endapo Trump atatekeleza kitisho chake cha kuziwekea vikwazo vya ushuru, huku Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent, akionya kuwa kisasi hicho hakitakuwa "jambo la busara."

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii