Katika kuhakikisha kikosi cha Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba Sports kinarejea kwenye ubora wa juu timu hiyo imemtambulisha rasmi, Ismael Toure na tayari nyota huyo yuko nchini kwa ajili ya kukitumikia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.“Ni kweli tunaendelea kuboresha kikosi chetu, tumefanya mchakato huu kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu wetu,” Ahmed All, Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba amesema.
Sambamba na hilo jana pia ilimtambulisha beki, Nickson Kibabage, kutoka Singida Black Stars ambapo pia wanatajwa wako katika mazungumzo ya kiungo wake wa zamani, Clatous Chama akitokea Singida Black Stars.
Hata dirisha dogo la usajili lililotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), litafungwa rasmi Januari 30, mwaka huu.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime