KATIKA kisa cha kusikitisha Chifu wa Turbo Kaunti ya Uasin Gishu William Koros ameruhusu familia ya watoto saba mayatima kuwa ombaomba ili kupata karo ya kumpeleka mmoja wao kujiunga na Gredi ya 10.
Ambapo watoto hao wanatoka kijiji cha Kiplombe viungani mwa jiji la Eldoret na hivyo wameamua kuwa ombaomba ili kupata karo na pesa za kumtimizia Fidel Otieno mahitaji yake ili ajiunge na shule ya upili ya Kandie.
Licha ya kufanya vizuri kwenye Mtihani wa Gredi ya Tisa, KJSEA, Otieno amekosa Sh15,000 ambazo zinahitajika kama karo ya kila mwaka kujiunga na shule hiyo.
NA alipata alama 46 katika Shule ya Sekondari ya chini ya Emkoin Kaunti ya Uasin Gishu Mlezi wao Esther Akoth hufanya vibarua kujikimu na anasema amesaka msaada wa basari kwa wanasiasa lakini amezuiwa kuwaafikia.
Baadhi hata hutaka pesa kutoka kwake ili kumwezesha kufikia mbunge wa eneo hilo.
Wakati huo huo, Mahakama Kuu ya Kibera, imewahukumu wanadada wawili miaka 10 gerezani kwa kumuua Beatrice Wangui, ambaye alikuwa na umri wa miaka 20 pekee.
Mary Njeri na dadake Lilian Muihaki walipatikana na hatia baada ya mahakama kubaini adhabu waliyompa Wangui ilipita mpaka na kuwa kitendo cha uhalifu.
Wangui alikuwa mwanawe wa kike wa pili wa Njeri na mamake mtoto mwenye umri wa miaka miwili. Alikuwa akiishi Kibiria Dagoretti na mamake pamoja na jamaa zake hadi pale uhasama na taharuki ya kifamilia ilichangia aondoke Desemba 24, 2024.
Alirejea siku iliyofuata kumchukua mwanawe na akawaambia jamaa zake alikuwa akimpeleka kwa babake. Alipokosa kurejea kuliibuka taharuki na shaka miongoni mamake, shangaziye na jamaa zake.
Mnamo Desemba 28, Muhiaki alimhadaa arejee nyumbani kwa madai ya uongo kuwa mamake (Njeri) alikuwa amehusika kwenye ajali ya barabarani.
Baada ya kurudi, Wangui alifungiwa ndani ya nyumba akapigwa na mamake na shangazi yake na jamaa wao mwengine huku akiomba ahurumiwe.
Njeri, 42, na Muhiaki, walishtakiwa kwa mauaji ila wakalilia mahakama wahukumiwe kwa kuuwa bila kukusudia.
Akiwahukumu, mahakama ilisema sheria inatoa adhabu ya miaka 30 kwa mauaji lakini alikuwa amepunguza hadi miaka 10 na ikatoa amri watumikie kifungo hicho.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime