Waumini 163 watekwa nyara kanishani Nigeria

Makundi yenye silaha yawateka nyara waumini 163 wa Kikristo baada ya kuyavamia makanisha mawili katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria.

katika taarifa zilizotolewa Januari 19 mwaka huu zilisema kuwa washambuliaji hao waliyavamia makanisa hayo na kuwalazimisha waumini hao kuondoka nao kuelekea maporini.

Ripoti hizo zilithibitishwa na vyanzo mbalimbali akiwemo mkuu  wa kanisa chifu wa kijiji na Umoja wa Mataifa ambapo  polisi wa jimbo hilo ilikataa kuthibitisha matukio hayo ilipoombwa na shirika la habari la AFP.

Aidha mashambulizi hayo ya Jumapili ni ya hivi karibuni kabisa katika wimbi la utekaji nyara unaofanywa na magenge yaitwayo majambazi katika taifa hilo la magharibi ya Afrika ambao huwalenga Wakristo na Waislamu, kwa ajili ya kudai fedha za kikomboleo.

Hata hivyi mnamo mwezi Novemba magenge hayo yaliwateka zaidi ya wanafunzi na walimu 300 kutoka skuli moja ya Kikatoliki, ambapo 50 walifanikiwa kukimbia na wengine kuachiliwa kwa mikupuo miwili wiki kadhaa baadaye.


#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii