Venezuela yawaachia huru "wafungwa wa kisiasa"

Shirika kubwa zaidi la kutetea haki za wafungwa nchini Venezuela limesema kuwa makumi ya wafungwa wameachiwa huru mwishoni wa juma lililopita.

Tangazo hilo limetolewa katika wakati Marekani inaendelea kuitia kishindo serikali mjini Caracas kuwaachia watu wengi zaidi waliotiwa korokoroni wakati wa utawala wa rais aliyeondolewa madarakani kwa mabavu, Nicolas Maduro.

Mkuu wa shirika hilo la Foro Penal, Alfredo Romero, amearifu kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba kwa jumla watu 266 alowataja kuwa "wafungwa wa kisiasa" wameruhusiwa kutoka gerezani  tangu Januari 8 mwaka huu.

Wafungwa 100 kati ya hao wameachiwa ndani ya kipindi cha siku mbili zilizopita katika kile serikali ya rais wa mpya Delcy Rodríguez -- aliyekuwa makamu wa Maduro -- imekitaja kuwa ishara ya nia njema.

Maduro alikamatwa na makomandoo wa Marekani mnamo Januari 3 na kupelekwa Marekani ambako amefunguliwa mashtaka.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii