Watu 25 wameuawa mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo jana Jumapili baada ya wanamgambo wa kundi lenye mafungamano na lile linalojiita Dola la Kiislamu kufanya shambulizi kwenye jimbo la Ituri.
Hayo yameelezwa na asasi moja ya kiraia yenye makao yake kwenye jimbo la Ituri ambapo asasi hiyo imesema kuwa miongoni mwa waliouawa katika shambulizi hilo la kundi la ADF, ni pamoja na wanaume 15 waliochomwa moto wakiwa hai na wengine saba waliopigwa risasi kwenye kijiji cha Apakulu.
Aidha watu wengine watatu wameuliwa katika eneo la Walese Vonkutu. Kundi la ADF linaloendesha hujuma zake kwenye mpaka kati ya Kongo na Uganda limekuwa likiwaua raia kiholela mashariki mwa Kongo kwa miaka kadhaa sasa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime