Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 26 mwaka huu ameondoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Morogoro kwa kutumia Treni ya Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).
Katika safari hiyo Dkt. Mwigulu anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye Mkutano wa Mwaka wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa TAKUKURU kutoka mikoa yote nchini kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa majukumu yao, kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime