Jarida la Time la nchini Marekani limesema idadi ya watu waliouawa katika siku mbili pekee wakati wa maandamano ya wiki kadhaa nchini Iran inaweza kufikia watu 30,000.
Jarida hilo limeandika kuwa vikosi vya usalama viliwaua watu hao kati ya Januari 8 na 9 ambapo Iran ilishuhudia maandamano makubwa zaidi.
Ripoti ya jarida hilo ya Jumapili iliyowanukuu maafisa wakubwa wawili wa afya wa imeeleza kuwa idadi kubwa ya miili ya waliouwawa ilielemea uwezo wa mamlaka za Iran wa kuzishughulikia.
Idadi kubwa ya maiti zilizosambaa mitaani ilizidi uwezo wa mamlaka
Ripoti hiyo imeongeza kuwa mamlaka ziliishiwa mifuko ya kuhifadhi maiti na malori yalitumika kuzikusanya badala ya magari ya kubebea wagonjwa.
Maandamano ya kupinga hali ngumu ya Uchumi hasa mfumuko mkubwa wa bei yaliibuka mwishoni mwa mwezi Desemba lakini yaligeuka kuwa ya kisiasa yaliyolenga kuuondoa utawala wa sasa wa Iran.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime