Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa taarifa kuwa namba ya simu ya Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho Brenda Rupia iliyokuwa ikitumika kupokea michango kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa chama hicho imefungiwa na Kampuni ya Airtel Tanzania tangu Januari 19 mwaka huu.
