JKT Watangaza Mafunzo ya Kujitolea 2026, Usaili Kuanza Januari 26

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele ametoa wito wa kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2026.

Akimwakilisha Mkuu wa JKT Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena  Januari 20 mwaka huu Makao Makuu ya JKT Chamwino jijininDodoma amesema kuwa  usaili utaanza Januari 26 mwaka huu kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Brigedia Jenerali Mabena ameongeza kuwa vijana watakaoteuliwa kujiunga na mafunzo ya JKT wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Februari 27, 2026 hadi Machi 04 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Mabena amefafanua kuwa JKT halitoi ajira, pia halihusiki na kuwatafutia ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Kiserikali bali hutoa mafunzo yatakayosaidia Vijana kujiajiri mara baada ya kumaliza mkataba wao na JKT.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii