Watu 114 wameuwa nchini Sudan, baada ya kushuhudiwa kwa makabiliano makali kati ya wanajeshi wa wanamgambo wa RSF, Magharibi mwa jimbo la Darfur kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.
Madaktari wamethibitisha idadi ya mauaji hayo, wakati huu wanamgambo wa RSF wakiendelea kusonga ili kudhibiti eneo lote la Kordofan, karibu na mpaka wa nchi jirani ya Chad.
Ripoti zinasema shambulio la jeshi liliwauwa watu 51 katika mji wa Al-Zuruq, ambapo raia wa kawaida, walilengwa sokoni na wengine wakiwa katia makaazi yao.
Mji wa Al-Zuruq, ni ngome ya wanamgambo wa RSF na nyumbani kwa wanafamilia wa kiongozi wa kundi hilo Jenerali Hamdan Daglo, ambaye amepoteza wanafamilia wake wawili katika shambulio hilo.
Nao wanamgambo wa RSF wameshtumiwa kuwauawa watu 63 na kuwajeruhi wenhine 57 kufikia Ijumaa iliyopita katika eneo la Kernoi, ambapo makabiliano hayo yamesababisha watu zaidi ya 7,000 wameyakimbia makaazi yao ndani ya siku ya mbili.
Vita vya Sudan vilivyoanza Aprili 2023, vimesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine Milioni 11 kuyakimbia makaazi yao.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime