Elon Musk ametoa Internet bure Venezuela

Bilionea namba moja duniani Elon Musk ametoa bure huduma ya internet kwa wananchi wa Venezuela.

Ambapo huduma hii ametoa kuanzia january 3 hadi february 3 ikiwa ni juhudi za kuwaunga mkono wananchi wa nchi hiyo baada ya Rais wao kukamatwa nchini Marekani.

Hivyo basi unapaswa kukumbuka kuwa Elon alikuwa mshirika mkubwa wa Rais Donald Trump ambapo alikuwa mshauri mkuu wa Rais kwa ufanisi serikalini  (DOGE)lakini aliondoka baada ya kutokuelewana na Rais Trump.

Aidha mpaka sasa umeibuka mvutano mkubwa  kwa baadhi ya matajiri wakubwa duniani na kihoja kuhusiana na tukio la kukamatwa kwa Rais Maduro ambapo ameshtakiwa kwa makosa ya usafirishaji dawa za kulevya.

Hata hivyo Elon Musk muungaji mkono wa siasa za mlengo wa kushoto nchini Marekani anatajwa kuwa ni mmoja wa raia wenye ushawishi mkubwa duniani.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii