Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, limewakamata watuhumiwa watatu wa matukio tofauti ya mauaji na ukatili wa kijinsia yaliyotokea mkoani hapa akiwamo Helakumi Kacheli (50), akijaribu kujiua kwa kujikata koromeo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, limewakamata watuhumiwa watatu wa matukio tofauti ya mauaji na ukatili wa kijinsia yaliyotokea mkoani hapa akiwamo Helakumi Kacheli (50), akijaribu kujiua kwa kujikata koromeo.
Inadaiwa akitumia silaha kali, muda mfupi baada ya kumuua mke wake, kwa kitu chenye ncha kali, alikamatwa wakiwa shambani kwa kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema katika tukio la kwanza Helakimu, mkulima na mkazi wa kijiji cha Sesenga, wilayani Morogoro, alikamatwa Januari 4, 2026 kwa tuhuma za kumuua mkewe Sofina Alipisini (27) wakiwa shambani.
Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa huyo baada ya kutekeleza tukio hilo la mauaji alijaribu kujiua kwa kujikata koromeo, kwa silaha kali lakini aliokolewa na sasa anaendelea na matibabu akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Katika tukio jingine, Justine Thomas (42), mkazi wa kijiji cha Sogeambele k
Kata ya Bwakila Chini, wilayani Morogoro, anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua Machafu Masanja (42) baada ya ugomvi uliohusiana na mauzo ya mpunga bila ridhaa yake.
Kamanda Mkama amesema tukio hilo lilitokea Januari 5, 2026 katika Kijiji cha Sogeambele kilichopo Tarafa na Kata Bwakira Chini, wilayani Morogoro.
Wakati huohuo, Andrew Katanga (33), mkulima na mkazi wa Katindiuka Wilaya ya Kilombero anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa, kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14.
Kamanda Mkama amesema tukio hilo lililotokea Desemba 31, 2025 mtuhumiwa alidaiwa kufanya kitendo hicho cha ukatili wa kijinsia baada ya kumfungia mtoto huyo chumbani kwake na kumuingilia kinguvu.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime