Papa Leo anaongoza kikao chake cha kwanza cha baraza la maaskofu tangu achaguliwe kwenye nafasi hiyo mwaka jana kufuatia kifo cha mtangulizi wake Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV(14) ameanza awamu mpya ya uongozi wake kwa kukutana na makadinali kutoka kote duniani kwenye makao makuu ya kanisa hilo Vatican, akisisitiza haja ya Kanisa Katoliki kukabiliana na mabadiliko na changamoto za nyakati za sasa. Papa Leo XIV
Katika mkutano huo, Papa Leo ameonyesha kuwa kipaumbele chake ni utekelezaji kamili wa mageuzi ya Baraza la Pili la Vatican la miaka ya 1960, yaliyolenga kuliboresha na kulifungua Kanisa kwa ulimwengu wa kisasa.
Mkutano huo wa baraza la makadinali, wa siku mbili ni wa kwanza kufanywa na Papa Leo tangu achaguliwe Mei 2025 kufuatia kifo cha mtangulizi wake Papa Francis.
Papa Leo XIV awasili Uturuki na kisha ataelekea Lebanon
Makadinali wanaripotiwa kutaka kushirikishwa zaidi katika uongozi wa Kanisa, wakitaka mfumo wa uongozi wa pamoja zaidi. Wakati wa miaka 12 ya uongozi wake, Papa Francis alikabiliwa na ukosoaji kutoka ndani ya Kanisa, ambapo baadhi ya makadinali walimkosoa kwa mtindo wake wa uongozi wa misimamo mikali ambao uliwatenga makadinali.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime