Mwanaume ashikiliwa Mvomero kwa Kumng’oa Kinguvu Mwanawe

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia mwanaume mwenye umri wa miaka 33 mkazi wa eneo la Katindiuka, wilayani Mvomero, kwa tuhuma za kumwingilia kimwili mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 14.

Taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo ilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 31, 2025 ambapo mtuhumiwa alidaiwa kumfungia chumbani kwake mtoto huyo na kumwingilia kinguvu.

Polisi wanasema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea huku mtuhumiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii