Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjær, ameonyesha nia ya kurejea Old Trafford kuinoa klabu hiyo kama Kocha wa Muda (Caretaker) hadi mwisho wa msimu wa 2025/2026.
Kupitia taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Manchester United imeelezwa kuwa Solskjær yupo tayari kurejea bila kujali muda wa mkataba huku akilenga kusaidia klabu hiyo katika kipindi hiki cha mpito.
Hatua hiyo inakuja baada ya Ruben Amorim kufutwa kazi mapema Januari 05 mwaka huu jambo lililoilazimu klabu hiyo kuanza mchakato wa kutafuta kocha mpya wa kudumu.
Aidha Uongozi wa United umeamua kuahirisha uteuzi wa Kocha Mkuu wa kudumu hadi majira ya joto ili kumpata kocha atakayeiongoza timu hiyo kuanzia msimu wa 2026/2027.
Hata hivyo kwa sasa majukumu ya kuiongoza timu yameshikiliwa na Darren Fletcher, ambaye ataiongoza Manchester United kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Burnley.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime