Watu 29 wamefariki katika maandamano dhidi ya serikali Iran

Maandamano makubwa yanayoendelea nchini Iran yameingia wiki ya pili huku idadi ya watu waliopoteza maisha ikifikia 29, kwa mujibu wa taarifa za wanaharakati wa haki za binadamu.

Watu 29 wamefariki dunia katika maandamano yanayoendelea nchini Iran huku maandamano hayo yakiingia wiki yake ya pili.

Miongoni mwa walioripotiwa kupoteza maisha ni maafisa wawili wa vikosi vya usalama.

Mtandao wa haki za binadamu wenye makao makuu yake nchini Marekani, HRANA, umesema kuwa zaidi ya watu 1,200 wamekamatwa katika maandamano hayo ya kuipinga serikali.

Kwa mujibu wa wanaharakati, maandamano yameripotiwa katika angalau miji 88 katika siku za hivi karibuni na yameenea katika majimbo 27 kati ya 31 nchini humo.

Mapema jana Jumatatu, mahakama ya Iran ilitangaza kuwa itachukua hatua kali dhidi ya waandamanaji bila kuonyesha huruma.

Jaji Mkuu Gholam-Hossein ametoa onyo kwa wale aliowaita "wachochezi" huku akizitaja Marekani na Israel kama maadui wakuu wa wananchi wa Iran, kutokana na hatua ya nchi hizo kuonyesha mshikamano na waandamanaji.

 #10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii