Liam Rosenior Yupo Mbioni Kujiunga na Chelsea Kama Kocha Mkuu

Klabu ya Chelsea ipo hatua za mwisho kumtangaza Liam Rosenior kuwa Kocha Mkuu mpya wa kikosi hicho, baada ya pande zote kufikia makubaliano ya awali.

 Rosenior anatarajiwa kuchukua nafasi ya Enzo Maresca aliyefutwa kazi hivi karibuni kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Hivyo Kocha huyo raia wa England ambaye kwa sasa alikuwa akiinoa Strasbourg ya Ufaransa amethibitisha mwenyewe kuwepo kwa mazungumzo hayo huku akieleza kuwa yuko karibu kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani.

“Ninaweza kuthibitisha kuwa ninakaribia kuwa meneja mpya. Nitasaini mkataba na moja ya klabu kubwa zaidi duniani,” amesema Rosenior.

Aidha Kwa mujibu wa taarifa Rosenior ataondoka rasmi Strasbourg na kujiunga na The Blues mapema ili kuiongoza timu hiyo katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Charlton utakaochezwa Januari 10 ambapo anatarajiwa kusimama kama kocha mkuu wa muda huo.

Hata hivyo iwapo dili hilo litakamilika, Rosenior ataungana na Chelsea yenye makazi yake jijini London, akiwa na jukumu kubwa la kurejesha heshima na ushindani wa klabu hiyo katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii