Aliyekuwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro aliyekamatwa pamoja mkewe Cilia Flores wakati wa operesheni maalum iliyotekelezwa na vikosi vya Marekani anatarajiwa kufikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu, jijini New York, anakokabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na makosa ya kujihusisha na silaha.
Kabla ya kukamatwa kwake, Maduro amekuwa akishtumiwa na serikali ya Marekani kwa kuongoza biashara haramu ya kusafirisha dawa za kulevya nchini Marekani, kwa muda mrefu, madai ambayo anakanusha.
Wakati Maduro, akitarajiwa Mahakamani, rais Donald Trump amemwonya kiongozi wa mpito wa Venezuala Delcy RodrÃguez, atalipa gharama kubwa iwapo, atatenda kinyume na matakwa ya Marekani.
Kiongozi huyo mpya wa Venezuela, amesema yupo tayari kushirikiana na serikali ya Trump, ambapo amemtaka kiongozi huyo wa Marekani kushirikiana naye kwa heshima.
Trump akiwa safarini, kurejea kwenye Ikulu ya White House, amesisitiza kuwa Marekani kwa sasa inasimamia Venezuela, hasa ikilenga kudhibiti sekta ya nchi hiyo ya mafuta ambako kampuni za nchi yake zitakwenda Marekani kuwekeza.
Naye Waziri wa Mambo ya nje, Marco Rubio amesema Marekani haipo kwenye vita na Venezuela, lakini inapambana na wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime