Watu wote 40 waliokufa katika moto uliotokea kwenye baa wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya nchini Uswisi wametambuliwa na mamlaka za nchi hiyo.
Polisi nchini humo imesema vijana ndio waliokuwa wengi miongoni mwa wahanga, wakichangia zaidi ya nusu ya idadi ya vifo.
Moto huo uliotokea katika eneo la burudani la Crans-Montana, umetajwa kuwa miongoni mwa majanga mabaya zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Uswisi na imeacha huzuni kubwa kote nchini.
Mamia ya watu waliandamana katika msafara wa kimya kimya wakipita katika barabara za Crans-Montana kuwakumbuka wahanga wa moto huo. Moto huo pia ulisababisha majeraha ya watu wengine zaidi ya 100.
Kwa mujibu wa polisi, takriban watu 26 kati ya 40 waliopoteza maisha walikuwa na umri wa chini ya miaka 20, wakiwemo raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 14 na raia wa Uswisi mwenye umri sawa na huo.
Rais wa Uswisi Guy Parmelin ametangaza kuwa nchi hiyo itaadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezo mnamo siku ya Ijumaa ili kuwakumbuka wahanga wa janga hilo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime