Trump kukutana na kiongozi wa upinzani wa Venezuela Machado

Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado atakutana na rais wa Marekani Donald Trump wiki hii. Mkutano huo utafanyika wakati Venezuela ikikabiliwa na shinikizo kuhusu kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa.

Marekani imetangaza hapo jana Jumatatu kwamba mwanasiasa wa upinzani wa Venezuela, Maria Corina Machado, atakutana na Rais Donald Trump wiki hii huku shinikizo likiongezeka kwa uongozi wa mpito huko Caracas ili kuharakisha kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa.

Wakati huo huo, Venezuela ilitangaza kuwa imewaachilia huru watu 116 zaidi waliofungwa chini ya kiongozi wa zamani Nicholas Maduro - wengi wao kwa kushiriki katika maandamano baada ya uchaguzi uliopingwa wa 2024.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalitilia shaka idadi hiyo, na wanafamilia walidai kuachiliwa huru haraka kulikoahidiwa na Caracas chini ya shinikizo kutoka Marekani.

Jamaa wamekuwa wakipiga kambi magerezani kwa siku nyingi, wakizidi kuwa na wasiwasi huku wapendwa wao wakishindwa kuonekana.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na upinzani walisema ni wafungwa wapatao 50 pekee ndio wameachiliwa huru hadi sasa kati ya 800-1,200 ambao mashirika ya haki za binadamu yanakadiria wanashikiliwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii