Tukio hilo limetokea January 12, 2026 katika mtaa wa Ligula "A" kata ya Chuno halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa chanzo cha moto huo ni watoto hao kutumia moto wakati wakiua wadudi aina ya nyigu kabbla ya moto huo kushika kwenye nyumba hiyo ambayo inasemekana ni ya muda mrefu.
Kwa upande wake afisa oparesheni wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Mtwara Ambroce Ndunguru amethibitisha kutokea kwa ajali huku akieleza kuwa wamepata taarifa hiyo kupitia majirani.
Mmiliki wa nyumba hiyo ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani bwana Anselm Masumbuko hakuwa tayari kuzungumza na wanahabari.