Nchini Afrika Kusini kila ifikapo Disemba 16 huwa ni maadhimisho ya Siku ya Maridhiano kufuatia juhudi za upatanisho nchini humo zilizolenga kuleta uponyaji kutokana na madonda yaliyochochewa na sera za ubaguzi wa rangi kupitia michakato kama vile Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) kukuza umoja wa kitaifa na kushughulikia dhuluma za awali.
Aidha tume hiyo iliongozwa na Askofu Desmond Tutu kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa iliyoanzishwa mwaka 1995 ili kukuza umoja, uponyaji na ujenzi wa taifa kwa kuzingatia utaifa na mshikamano wa kijamii.
Hivyo basi Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyojikuta kwenye sintofahamu katika siku za karibuni baada ya maandamano yaliyogubikwa na ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu na kusababisha maafa kuanzia vifo na majeruhi na uharibifu mkubwa.
Hata hivyo Kisa hiki pia kimeacha mpasuko, maumivu na majeraha makubwa kwa kijamii katika baadhi ya familia.
Je, kwa kuangazia siku hii ya maridhiano, Tanzania na nchi nyingine za Afrika zinajifunza nini?
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime