Bunge la Zambia limepitisha jana kwa wingi wa kura mswaada wa kurekebisha vifungu vya katiba vinavyohusiana na uchaguzi ambavyo upinzani unadai vitamsaidia Rais Hakainde Hichilema katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Baada ya kura hiyo iliyoungwa mkono na wabunge 131 na kupingwa na wawili, waziri wa sheria Princess Kasune alisema kuwa hayo ni maagano na watu wa Zambia katika juhudi za kukuza haki.
Mbunge Francis Kapyanga kutoka chama cha upinzani cha Patriotic Front (PF) amesema "hatahalalisha kitu kisicho halali".
Wanasiasa wa upinzani, mashirika ya kiraia na makundi ya makanisa yalikuwa yamepigia debe kupingwa kwa muswada huo nambari 7 na kusema uliharakishwa kupitishwa bungeni.
Marekebisho kwenye muswada wa sheria
Mswaada huo pia ulitaka kufanyia marekebisho vifungu vya katiba ya taifa hilo la kusini mwa Afrika lenye utajiri wa shaba hasa kwa kuongeza idadi ya viti vya wabunge maalumu pamoja na kutenga viti 40 kwa wanawake, vijana na walemavu, na kuhitimisha ukomo wa mihula miwili ya miaka mitano kwa mameya.
Mswaada huo unapaswa kusainiwa na Rais Hichilema kuwa sheria.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime