Kamati Mambo ya Nje Bunge la Marekani kutembelea Tanzania

MWENYEKITI wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani, na Mbunge machachari wa Chama cha Republican katika Jimbo la Florida, Brian Mast, amepokea mwaliko wa kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.

Hayo yanajiri ikiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo, anafanya ziara rasmi ya kikazi jijini Washington, D.C nchini Marekani, ambako mionhoni mwa viongozi wa kwanza aliokutana nao ni mwenyekiti huyo wa kamati ya mambo ya nje ya bunge

Kwa mujibu wa taarifa ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC, katika ziara hiyo ya Balozi Kombo atakukutana pia na wadau mbalimbali muhimu katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Marekani. 

"Wakati akiwa nchini Marekani, Waziri pamoja na masuala mengine, atakutana pia na kufanya mazungumzo ya kina na serikali na wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani," imesema sehemu ya taarifa hiyo. 

Imeelezwa kuwa Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani pia wamekubaliana mambo kadhaa na Balozi Kombo juu ya uimarishaji mahusiano na Tanzania.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii