Uamuzi mdogo kesi ya ghorofa la Kariakoo kutolewa leo

Uamuzi mdogo wa kesi ya kuporomoka kwa ghorofa la Kariakoo, iliyosababisha vifo na madhara makubwa kwa wananchi, unatarajiwa kutolewa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo imefunguliwa na Daftari Swai na wenzake 49, chini ya uongozi wa wakili Peter Madeleka, ambao wanaitaka mahakama iamuru walipwe fidia inayozidi shilingi bilioni 40. Wanadai kuwa walipata hasara kubwa kufuatia kuporomoka kwa jengo hilo mwaka 2025, ikiwamo kupoteza mali, kuumia pamoja na kupata athari mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Katika shauri hilo, walalamikaji wanamshataki mmiliki wa jengo, kampuni iliyolijenga, wadau waliohusishwa na mradi huo pamoja na mamlaka zinazodaiwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa usimamizi wa ujenzi.

Uamuzi wa leo unafuatiliwa kwa karibu na wananchi, hususan wakazi wa Kariakoo na familia zilizoathirika na tukio hilo, kutokana na uzito na athari kubwa iliyosababishwa na ajali hiyo katika jamii.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii