Rais wa Marekani Donald Trump amesema atasitisha kwa muda uhamiaji kutoka nchi alizozitaja kama “masikini,” ikiwa ni siku moja baada ya raia wa Afghanistan kudaiwa kuwapiga risasi na kuwaua wanajeshi wawili wa ulinzi wa taifa hilo.
Trump alisema hatua hii imechukuliwa baada ya raia wa Afghanistan kudaiwa kuwapiga risasi walinzi wake wawili Sarah Beckstrom, mwenye umri wa miaka 20 na mwanachama wa Jeshi la Taifa walio fariki dunia kutokana na majeraha waliyopata baada ya kushambuliwa mjini Washington huku askari mwingine Andrew Wolfe (24) akijeruhiwa vibaya na bado amelazwa hospitalini.
Aidha Kupitia mtandao wake wa kijamii Trump amesema kuwa atabatilisha maombi ya mamilioni ya wahamiaji yaliyoidhinishwa na utawala wa rais wa zamani Joe Biden hatua inayoongeza kasi ya msimamo wake mkali dhidi ya wahamiaji.
Hata hivyo Maafisa wa ujasusi wameanzisha uchunguzi wa tukio hilo na wamemtambua mshukiwa kuwa ni Rahmanullah Lakanwal, kijana wa miaka 29 aliyewahi kufanya kazi na kikosi cha Marekani cha Zero Units nchini Afghanistan kikosi kinachoshirikiana na shirika la ujasusi la Marekani (CIA) katika operesheni za kupambana na ugaidi ambapo hadi sasa, haijafahamika sababu ya mshukiwa kutekeleza shambulio hilo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime