Polisi wa Ujerumani walalamikiwa kutumia nguvu kupita kiasi

Polisi nchini Ujerumani wameshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi na waandamanaji baada ya kushambulia na kutumia virungu dhidi ya kundi la waandamanaji waliokuwa wakipinga ufashisti mwishoni mwa wiki.

Muungano wa maandamano Widersetzen, uliokuwa ukipinga kuanzishwa kwa shirika la vijana linalohusiana na chama cha mrengo mkali wa kulia Alternative für Deutschland (AfD), ulishtumu polisi kwa ukatili dhidi ya waandamanaji katika jiji la Giessen, magharibi mwa Ujerumani.

Lakini polisi walisema juhudi zao zililenga kuzuia vurugu kati ya makundi ya kisiasa yanayopingana. Makumi ya maelfu walikusanyika Jumamosi, wakizuia barabara zinazoingia katika mji wa chuo kikuu wenye wakazi takriban 90,000 kwa lengo la kuvuruga kuanzishwa kwa tawi la vijana wa mrengo mkali wa kulia.

Kimsingi polisi nchini Ujerumani wameshutumiwa mara kadhaa kwa kutumia nguvu kupita kiasi katika maandamano ya kuunga mkono Palestina, mazingira na kupinga ufashisti, ambapo waandamanaji wamejeruhiwa.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii