Jeshi la Israel limetoa taarifa kuwa Jumapili ya Novemba 30 mwaka huu limewaua zaidi ya wapiganaji 40 wa Kipalestina katika operesheni dhidi ya mitandao ya mahandaki karibu na Rafah Ukanda wa Gaza wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makumi ya wapiganaji wa Hamas wanadaiwa kujificha kwenye mahandaki ya kusini mwa Gaza, chini ya maeneo yanayodhibitiwa na jeshi la Israel.
Aidha Vyanzo kadhaa vilivyozungumza na AFP siku ya Alhamisi vilisema mazungumzo yanaendelea kuhusu hatima ya wapiganaji waliobaki katika mtandao wa mahandaki ya kusini mwa Gaza.
Hivyo Jumatano Hamas ilizitaka nchi zinazoshiriki mazungumzo hayo zishinikize Israel kuwaruhusu wapiganaji kupata njia salama ikiwa ni mara ya kwanza kundi hilo kukiri hadharani hali hiyo.
Hata hivyo Kwa zaidi ya siku 40 sasa, wanajeshi wa Israel wamekuwa wakifanya operesheni mashariki mwa Rafah kwa lengo la kuvunja njia za mahandaki zilizobaki na kuwaangamiza wapiganaji wanaojificha humo.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime