Wasichana 12 waokolewa kutoka kwa watekaji

Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa wasichana 12 waliotekwa nyara na kundi la kigaidi la Islamic State West Africa Province (ISWAP) katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Wasichana hao waliokadiliwa kuwa na  umri kati ya miaka 15 na 20 walitekwa nyara wiki moja iliyopita walipokuwa wakifanya kazi shambani katika wilaya ya Mussa Borno maeneo ambayo yako mbali na miji mikuu na ambayo mara nyingi hulengwa na makundi yenye mafungamano na makundi makubwa ya kigaidi.

Kwa mujibu wa Jeshi la Nigeria waathiriwa hao waliokolewa Novemba 29 mwaka huu  na wamepelekwa kituo cha kijeshi kupokea huduma za kitabibu na usaidizi wa kiakili kabla ya kuruhusiwa kurejea majumbani kuungana na familia zao.

Aidha taarifa hizo zimepokelewa kwa faraja katika jamii hasa ikizingatiwa madhara makubwa yaliyosababishwa na tukio hilo.

Hivyo uvamizi huo unatokea wakati ambapo Nigeria inakabiliwa na hali tete ya usalama katika maeneo ya kati na kaskazini, ikiwemo mashambulizi ya makundi ya kihalifu, wizi wa mifugo na utekaji nyara, hususan katika majimbo ya kaskazini magharibi.

Ingawa katika wiki za karibuni makundi ya wahalifu yamevamia vijiji kadhaa na kuteka watu wengi katika majimbo ya Kebbi, Niger na Kwara, ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa shule.

Hata hivyo eneo hilo limekuwa kitovu cha mzozo wa takriban miaka 16 unaohusisha makundi ya kijihadi, ikiwemo Boko Haram na ISWAP 

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii