IEBC yaonya wapiga kura dhidi ya kupiga picha za karatasi zenye alama za kupigia kura

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka imewatahadharisha wapiga kura katika maeneo ambayo uchaguzi mdogo unafanyika dhidi ya upigaji picha wa karatasi za kupigia kura zilizowekwa alama.

Tume hiyo ilionya kuwa wapiga kura watakaopatikana wakishiriki picha za kura zilizowekwa alama watakamatwa na kushtakiwa kwa kufanya makosa ya uchaguzi. Mawakala wa vyama pia walitakiwa kuzingatia kwa dhati sheria na itifaki za upigaji kura. 

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii