Mtwara Kliniki ya ardhi yatoa hamasa kwa wananchi kumiliki ardhi

Kliniki ya Ardhi inayoendelea mitaa ya Mbae Mashariki na Likombe katika manispaa ya Mtwara- Mikindani mkoani Mtwara imetoa muitikio kwa wananchi wa mtaa mitaa hiyo  kufuatilia masula ya ardhi ikiwemo  umilikishwaji mashamba.

Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Makao Makuu, Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mtwara na Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa ya Mtwara-Mikindani inaendelea na utoaji huduma za sekta ya ardhi kupitia Kliniki ya Ardhi iliyoanza  Novemba 17 mwaka huu katika Ofisi za Serikali za Mitaa ya Mbae na Lilombe katika manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Mkazi wa Mtaa wa Mbae Mashariki kata ya Ufukoni  Mwl. Yusuph Suleiman Ching'alang'ata amesema, huduma za ardhi zinazotolewa kupitia kliniki ya ardhi ni chachu inayopelekea wananchi wengi kuwa na mwitikio wa kufuatilia mauala yanayohusu ardhi ikiwemo umilikishwaji wa Mashamba.

Mwl. Ching'alang'ata amesema hayo mapema Novemba 24 mwaka huu katika ofisi ya serikali ya mtaa wa Mbae mara baada ya kukabidhiwa Hati Miliki ya Ardhi na Kamishna Msaidizi Utawala wa Ardhi Bi. Hellen Philip wakati wa kliniki ya ardhi katika mtaa huo.

" Kwa kweli huduma zinazotolewa kupitia kliniki hii ya ardhi hapa Mbae zinatutia moyo na kutupa mwitikio wa kufutilia masuala yote yanayohusu ardhi ikiwemo umilikishwaji mashamba amesema Ching'alang'ata.

Mwl. Ching'alang'ata amekiri kuwa uwepo wa kliniki ya ardhi katika mtaa wa Mbae umesogeza huduma za sekta ya ardhi karibu na wananchi jambo alilololieleza limewasaidia kupata huduma kwa haraka zaidi.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea na kliniki maalum za ardhi katika maeneo mbalimbali nchini Baadhi ya maeneo ambayo kliniki hizo maalum zimefanyika ni Chalinze mkoa wa Pwani, Nzega Tabora, Mbarali Mbeya kata ya Muriet Arusha na wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe. 

Hata hivyo huduma zinazotolewa katika Kliniki za Ardhi ni pamoja na utoaji hati milki za ardhi papo kwa hapo kwa waliokamilisha taratibu za umiliki, utoaji elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya mfumo wa utoaji huduma za ardhi kidigiti (e-ardhi), uhakiki na utambuzi wa viwanja vya wananchi uwandani, utoaji namba .

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii