Mafuriko yazidi kuitesa Sri Lanka vifo vyaongezeka

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Sri Lanka imezidi na kufikisha idadi ya watu 330 huku nchi hiyo ikikabiliana na mojawapo ya maafa mabaya zaidi ya hali ya hewa ambayo hayakuwahi kutokea kwa miaka mingi.

Kwa mujibu wa ripoti iliyoripotiwa nchini humo Zaidi ya watu 200 bado hawajulikani walipo na nyumba 20,000 zimeharibiwa na kupeleka watu 108,000 kwenda kuishi katika makazi ya muda ya serikali.

Aidha Maafisa wamesema kuwa karibu theluthi moja ya nchi haina umeme na maji ya bomba huku hali ya hatari ikitangazwa, baada ya kimbunga cha Ditwah.

Rais Anura Kumara Dissanayake amesema ni janga la asili lenye changamoto nyingi katika historia ya nchi hiyo, na uharibifu ni mkubwa sana.

Maagizo ya kuhama yametolewa katika baadhi ya maeneo huku viwango vya maji vya Mto Kelani vikiendelea kupanda kwa kasi.

Idadi kubwa zaidi ya vifo iliripotiwa Kandy na Badulla, ambapo maeneo mengi hayafikiki.

Serikali imetoa ombi la msaada wa Kimataifa na kuwataka raia wa Sri Lanka walio nje ya nchi kuchangia pesa kusaidia jamii zilizoathirika.

Kimbunga Ditwah kiliikumba pwani ya mashariki ya kisiwa hicho siku ya Ijumaa lakini tangu wakati huo kimeondoka nchini.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii