Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Samuel Kijanga, amewataka wanafunzi wa vyuo kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na badala yake kuitumia kwa manufaa ya kitaaluma na maendeleo ya Taifa.
Akizungumza na wanachuo wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Waislam kilichopo mkoani humo, ACP Kijanga aliainisha madhara ya matumizi mabaya ya mitandao, yakiwemo kusambaza taarifa za upotoshaji zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
Amesisitiza umuhimu wa kufuta au kupuuza taarifa zisizo na maadili, zenye mwelekeo wa uchochezi, na kuhimiza wanachuo kuwa mstari wa mbele kulinda maadili na amani ya Taifa kupitia matumizi sahihi ya teknolojia.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime